Waziri Mchengerwa aongoza kikao cha ujumbe wa Tanzania, Birmingham Uingereza
Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohammed Mchengerwa ameongoza kikao cha maandalizi ya ujumbe wa Tanzania katika kikao cha Mawaziri wa Michezo wa Jumuiya ya Madola kitakachoanza leo Julai 26 mjini Birmingham, Uingereza. Kikao hicho ni maandakizi mahususi kabla ya uzinduzi rasmi wa mashindano ya michezo ya Jumuiya ya Madola ya mwaka huu yanayofanyika nchini Uingereza huku Tanzania ikiwa imeshiriki katika michezo hiyo. Katika mashindano hayo kwa mara ya kwanza Serikali imetoa motisha kubwa kwa wachezaji watakaofanya vizuri na kurejea na tuzo nchini. Mhe. Mchengerwa amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha michezo inatumika kikakamilifu kuitangaza Tanzania kimataifa. Aidha, amesema michezo ni ajira na uchumi mkubwa ambapo amesisitiza wachezaji wote kuwa wazalendo kujituma kufa na kupona kwa ajili ya taifa la Tanzania. Amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan za kuleta mapind...